main dental handpieces

Je, handpieces zako zinaharibika mara kwa mara? Hizi hapa Sababu 5 kuu (Na jinsi ya kuzizuia)

Je, Handpiece Zako Zinaharibika Mara kwa Mara?

Hizi Hapa Sababu 5 Kuu na Jinsi ya Kuzizuia

Dental handpiece / dental clinic equipment

Dental handpiece ni moja ya vifaa vinavyofanya kazi kubwa zaidi ndani ya kliniki ya meno. Lakini kliniki nyingi hujikuta zikibadilisha handpiece mara kwa mara — si kwa sababu ya ubora mdogo, bali kutokana na makosa ya kawaida ya matengenezo ambayo yanaweza kuzuilika.

1. Poor Lubrication Habits
2. Poor Drainage of Dental Air Compressors
3. Delayed Air Filter Replacement
4. Allowing Running Tap Water Into Handpieces
5.Excessive Air Pressure
Sababu 1

Poor Lubrication habits (Kutolubricate Handpiece ipasavyo)

Lubricate baada ya kila Mgonwa/Mteja usisubiri mpaka mwisho wa siku pekee

Moja ya sababu kubwa zinazoharibu handpiece mapema ni kutofanya lubrication ipasavyo. Kanuni rahisi ni hii: lubricate handpiece baada ya kila mgonjwa au procedure.

Kliniki nyingi zina handpiece chache kwa kila daktari, hivyo handpiece zilezile hutumika siku nzima bila lubrication ya kutosha kati ya mgonjwa mmoja na mwingine. Hali hii husababisha:

  • Bearing kuharibika
  • Handpiece kupata moto kupita kiasi
  • Turbine kuchoka mapema
  • Kupungua kwa speed na nguvu ya handpiece
  • Kupungua kwa maisha ya handpiece
  • Suluhisho: Hii lazima iwe sehemu ya kawaida ya kazi za dental assistants na wauguzi baada ya kila procedure. Kabla ya mgonjwa mwingine kuingia, lubrication inapaswa kuwa sehemu ya lazima ya post-op activities na si jambo la hiari. Mafunzo mazuri ya staff huokoa gharama kubwa za matengenezo na za kuendesha klinik.
Sababu 2

Poor drainage habits of dental air compressors (Kutodrain Compressor kwa wakati)

Adui mkubwa wa handpiece zako

Compressor isipodrainiwa vizuri, maji hukusanyika ndani ya tank na kuingia kwenye mfumo wa hewa wa dental chair. Baadaye unyevu huu hufika kwenye air lines za handpiece.

  • Kutu ndani ya handpiece
  • Corrosion ya internal compartments
  • Kupungua kwa suction efficiency
  • Slow-speed suction kufanya kazi vibaya
  • Water leakage kwenye dental chair

Ushauri: Drain compressor kila siku au kulingana na matumizi ya kliniki.

Sababu 3

Kutobadilisha Air Filters kwa Wakati

Filter ndogo, hasara kubwa

Air filter hulinda handpiece dhidi ya vumbi,na unyevu kutoka kwenye air compressor. Filter zisipobadilishwa kwa wakati hupelekea, uchafu kuingia kwenye air lines na kupunguza air pressure. Na hii upelekea

  • Air pressure hupungua
  • Bearings kushindwa kuzunguka vizuri
  • Turbine na suction kupoteza nguvu
  • Handpiece huwa na kelele
  • Handpiece hufanya kazi chini ya kiwango

Muda wa kubadilisha: Badilisha air filters kila miezi 3–6, au mapema zaidi kwa kliniki zenye wagonjwa wengi.

Dental Chair Air Filters / Compressor Filters

Dental Chair Air Filter

Price: 40,000 Tsh

Click here to get the product at discounted price
Sababu 4

Kuruhusu Running Water Kuingia Kwenye Handpiece

Siyo kila maji yanafaa kwa dental unit

Dental chair nyingi zina toggle switch ya kubadilisha kati ya bottle water system na running tap water (maji ya bomba). Tatizo hutokea pale mtu anapobadilisha kwa bahati mbaya au kwa makusudi kutoka kutumia botle water kwenda kutumia maji ya bomba. Hii hupelekea

  • Impurities na sediments kuingia kwenye mirija ya maji ndani ya dental chair
  • Minerals husababisha scaling
  • Internal water lines huziba
  • Cooling system huathirika
  • Corrosion huongezeka ndani ya mfumo

Ushauri: Tumia bottle water system yenye maji safi na badilisha water filters kila baada ya miezi 3-6

Sababu 5

Kutumia Air Pressure Kubwa Kupita Kiasi

Pressure kubwa = uharibifu wa haraka

Kliniki nyingi huharibu handpiece bila kujua kwa kutumia air pressure kubwa sana. Unapokanyaga foot pedal hadi mwisho, pressure ya handpiece inapaswa kuwa:

0.2 – 0.3 MPa

    matumizi ya upepo uliozidi kiwango hichi husababisha chanagmoto zifuatazo ndani ya handpiece yako:
  • Bearing failure
  • Turbine damage
  • Hanpiece Vibration
  • Overheating
  • Handpiece kuharibika mapema

Pressure kubwa haimaanishi performance nzuri zaidi, bali ina maana ya uharibifu wa haraka zaidi.

Pressure Gauge

Pressure Gauge

Price: 25,000 Tsh

Ni muhimu kifaa hiki kuwepo kwenye dental chair yako ili kukuwezesha kufuatilia pressure ya upepo kwa urahisi na kuhakikisha handpiece zako zinafanya kazi ndani ya pressure inayoshauriwa.

Click here to get the product at discounted price

Ushauri wa Mwisho

Handpiece nyingi haziharibiki kwa sababu ya ubora mdogo wa bidhaa. Zinaharibika zaidi kwa sababu ya poor maintenance na matumizi yasiyo sahihi ya vifaa.

Kliniki inayoboreshwa kwenye lubrication, drainage ya compressor, kubadilisha filters, ubora wa maji pamoja na setting sahihi ya air pressure itaokoa gharama kubwa za matengenezo na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa.

Good Maintenance si Gharama — Ni Uwekezaji.

Karibu hapa Apex Dental kujipatia handpiece kwa bei nafuu, zikiwa na warranty ya mwaka mzima. Na kwa vile tunajishughulisha pia na matengenezo ya vifaa vya dental clinic, huduma ya utengenezaji itapatikana kwa haraka pale inapohitajika.

Click Here to View All Our Products Fuata Apex Dental Shop Instagram

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *