Dental handpiece ni moja ya vifaa vinavyofanya kazi kubwa zaidi ndani ya kliniki ya meno. Lakini kliniki nyingi hujikuta zikibadilisha handpiece mara kwa mara — si kwa sababu ya ubora mdogo, bali kutokana na makosa ya kawaida ya matengenezo ambayo yanaweza kuzuilika.
Poor Lubrication habits (Kutolubricate Handpiece ipasavyo)
Lubricate baada ya kila Mgonwa/Mteja usisubiri mpaka mwisho wa siku pekee
Moja ya sababu kubwa zinazoharibu handpiece mapema ni kutofanya lubrication ipasavyo. Kanuni rahisi ni hii: lubricate handpiece baada ya kila mgonjwa au procedure.
Kliniki nyingi zina handpiece chache kwa kila daktari, hivyo handpiece zilezile hutumika siku nzima bila lubrication ya kutosha kati ya mgonjwa mmoja na mwingine. Hali hii husababisha:
- Bearing kuharibika
- Handpiece kupata moto kupita kiasi
- Turbine kuchoka mapema
- Kupungua kwa speed na nguvu ya handpiece
- Kupungua kwa maisha ya handpiece Suluhisho: Hii lazima iwe sehemu ya kawaida ya kazi za dental assistants na wauguzi baada ya kila procedure. Kabla ya mgonjwa mwingine kuingia, lubrication inapaswa kuwa sehemu ya lazima ya post-op activities na si jambo la hiari. Mafunzo mazuri ya staff huokoa gharama kubwa za matengenezo na za kuendesha klinik.
Poor drainage habits of dental air compressors (Kutodrain Compressor kwa wakati)
Adui mkubwa wa handpiece zako
Compressor isipodrainiwa vizuri, maji hukusanyika ndani ya tank na kuingia kwenye mfumo wa hewa wa dental chair. Baadaye unyevu huu hufika kwenye air lines za handpiece.
- Kutu ndani ya handpiece
- Corrosion ya internal compartments
- Kupungua kwa suction efficiency
- Slow-speed suction kufanya kazi vibaya
- Water leakage kwenye dental chair
Ushauri: Drain compressor kila siku au kulingana na matumizi ya kliniki.
Kutobadilisha Air Filters kwa Wakati
Filter ndogo, hasara kubwa
Air filter hulinda handpiece dhidi ya vumbi,na unyevu kutoka kwenye air compressor. Filter zisipobadilishwa kwa wakati hupelekea, uchafu kuingia kwenye air lines na kupunguza air pressure. Na hii upelekea
- Air pressure hupungua
- Bearings kushindwa kuzunguka vizuri
- Turbine na suction kupoteza nguvu
- Handpiece huwa na kelele
- Handpiece hufanya kazi chini ya kiwango
Muda wa kubadilisha: Badilisha air filters kila miezi 3–6, au mapema zaidi kwa kliniki zenye wagonjwa wengi.
Price: 40,000 Tsh
Click here to get the product at discounted price